RATIBA ya TRENI January 27-28, 2025

Filed in Habari by on January 26, 2025 0 Comments
     
RATIBA ya TRENI January 27-28, 2025

RATIBA ya TRENI January 27-28, 2025

RATIBA ya TRENI January 27-28, 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapenda kuuarifu umma kuwa ratiba ya safari za treni kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, zitaendelea na ratiba yake kama ilivyopangwa licha ya baadhi ya barabara muhimu kufungwa kufuatia mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika, unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Januari 27-28, 2025.

Shirika hilo linawaomba abiria husika kupanga vizuri namna ya kufika mapema stesheni wanazotarajia kupandia treni hususani kituo cha Magufuli jijini Dar es Salaam na cha Samia jijini Dodoma, ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Katika hatua nyingine kufuatia kufungwa kwa barabara tajwa na Jeshi la Polisi Tanzania, TRC inapenda kuuarifu umma na abiria wanaotarajia kusafiri kati ya Dar es Salaaam na Dodoma January 27 na 28, 2025 kuwa treni zote ikiwemo ya Express, zitasimama kupakia na kushusha abiria katika kituo cha Pugu na kwamba utaratibu huu utahusu pia abiria wa kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!