SERIKALI Kuongeza Mikopo ya Wanafunzi wa Stashahada

SERIKALI Kuongeza Mikopo ya Wanafunzi wa Stashahada
SERIKALI Kuongeza Mikopo ya Wanafunzi wa Stashahada
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali imejipanga kuongeza wigo wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati vinavyotoa stashahada lengo ni kuongeza idadi ya wataalamu.
Utoaji wa mikopo katika ngazi za stashahada kwa wanafunzi wa ngazi hiyo ya elimu ulianza mwaka 2023/24, kwa fani sita za kipaumbele ambazo zina uhitaji mkubwa wa wataalamu ambazo ni afya na sayansi shirikishi, ualimu wa hisabati.
Fani nyingine ni fizikia na mafunzo ya amali, uhandisi na nishati, madini na sayansi ya ardhi, kilimo na mifugo ambapo Sh48 bilioni zilitengwa kwaajili ya wanafunzi 8,000.
Akizungumza Jumanne ya Aprili 29,2025 wakati wa kufungua mkutano Mkuu wa Shirika la Mtetezi wa Mama, Profesa Mkenda alisema Kuwa Serikali ya awamu ya sita, imefanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Elimu ikiwamo ya kutoa mikopo kwa ngazi ya stashahada.
Aliongeza kuwa katika kuzalisha vijana wenye ujuzi, Serikali iliamua kuanza kutoa mikopo ngazi ya stashahada kwa kozi za kipaumbele na mpango wa sasa ni kuongeza wigo wa kozi zitakazonufaika na mpango huo.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
