SERIKALI Kutangaza Ajira Mpya 45000 Kada Mbalimbali

SERIKALI Kutangaza Ajira Mpya 45000 Kada Mbalimbali
SERIKALI Kutangaza Ajira Mpya 45000 Kada Mbalimbali
Serikali imesema kabla ya mwaka huu wa fedha 2025/2026 kuisha itakuwa imetangaza nafasi za ajira mpya 45,000 kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake unafanyika.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni leo Jumanne tarehe 27 May 2025 na Naibu Waziri, Deus Sangu ambaye amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26 Serikali imeidhinisha jumla ya nafasi 41,500 za ajira mpya kwa kada mbalimbali ambazo zitawalenga kuajiri wahitimu stahiki.
Naibu waziri huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga ambaye ametaka kujua Serikali ina mpango gani wa kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo nchini.
Sangu amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imetoa nafasi 47,404 za ajira mpya kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake unaendelea kupitia sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma na mamlaka nyingine na wasailiwa kutoka vyuo mbalimbali waliofaulu wamepangiwa vituo vya kazi.
“Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali inatarajia kutoa ajira mpya 45,000 kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake utafanyika kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha,” amesema naibu waziri.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
