SERIKALI Yaipa Simba ndege ya Kuifuata RS Berkane Fainali ya CAF 2025

Filed in Michezo by on May 9, 2025 0 Comments
     
SERIKALI Yaipa Simba ndege ya Kuifuata RS Berkane Fainali ya CAF 2025

SERIKALI Yaipa Simba ndege ya Kuifuata RS Berkane Fainali ya CAF 2025

SERIKALI Yaipa Simba ndege ya Kuifuata RS Berkane Fainali ya CAF 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Palamagamba Kabudi akiwa Bungeni Jijini Dodoma imetangaza kuipa Simba ndege kuelekea nchini Morocco kwenye mchezo wa Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Baada ya mafanikio makubwa ya Simba na sasa inaingia kwenye mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho linaloandaliwa na CAF, Simba inakwenda Morocco kupambana na RS Berkane na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dr Samia imefanya maamuzi ya kutoa ndege itakayoipeleka Klabu ya Simba Morocco kwaajili ya mchezo huo”

Maamuzi hayo yamefanyika kama sehemu ya jitihada za Serikali za kuipunguzia Simba umbali wa safari na uchovu Simba kwenda Morocco kwa ndege ya abiria kungewafanya wazunguke na kutumia muda mwingi njiani kutokana na kulazimika kupita nchi tofautitofauti kwaajili ya kuunganisha ndege.

Ikumbukwe kuwa klabu ya Simba imekuwa na ratiba ngumu kuelekea mchezo huo wakilazimika kucheza mechi 4 kwa siku 10 kabla ya kusafiri kuwafuata RS Berkane huku mchezo wa mwisho watacheza May 11 dhidi ya KMC na mchezo wa kwanza wa Fainali umepangwa kuchezwa May 17 hivyo ndege hiyo itakuwa nafuu kubwa kwa Simba SC.

Aidha hii sio mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzisaidia usafiri timu za Tanzania katika michezo ya Kimataifa ili kuhakikisha zinafanya vizuri kwani hata baada ya Yanga kufuzu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika tarehe 3 June 2023 dhidi ya USM Alger alitoa ndege iliyoipeleka timu hiyo Algeria na kuirudisha Dar es salaam.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *