Shindano la Ubunifu wa Nembo ya Ofisi ya Msajili wa Hazina

Filed in Ajira by on February 17, 2025 0 Comments
     
Shindano la Ubunifu wa Nembo ya Ofisi ya Msajili wa Hazina

Shindano la Ubunifu wa Nembo ya Ofisi ya Msajili wa Hazina

Shindano la Ubunifu wa Nembo ya Ofisi ya Msajili wa Hazina

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Ofisi ya Msajili wa Hazina inapenda kuwaalika wabunifu wa nembo na wananchi kwa ujumla kushiriki katika shindano la kubuni Nembo rasmi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) ambayo itazingatia dira, dhima na majukumu ya Ofisi.

Nembo hiyo inatakiwa iwe rahisi kutambulika na kusomeka iwapo itatumika katika maeneo tofauti kama vile Vyombo vya Usafiri, Mabango, Majengo, Tovuti, Mavazi, Mikoba, “Business Card“, matangazo ya Televisheni na mitandao ya kijamii pamoja na machapisho mengine.

Nembo iwe na jina la rangi inayovutia na kuleta maana kwa kuzingatia dira, dhima na majukumu ya Ofisi na kuambatanisha namba za rangi zinazotambuliwa na kompyuta “color code” (RGB/CMYK).

Vigezo vitakavyotumika katika kumchagua Mshindi

  • Urahisi wa Kutambulika: Nembo inapaswa kuwa wazi na inayoweza kutambulika kwa urahisi kwa matumizi mbali mbali kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 2.
  • Maelezo ya Maandishi na maana yake: Ubunifu huu unapaswa kuambatana na maelezo ya maandishi ya maana na vipengele vyake; yaani maana ya kila alama iliyopo kwenye nembo.
  • Uhalisia wa Ubunifu: Ubunifu utakaowasilishwa ni lazima uwe halisi na uwe umebuniwa na aliyetuma ubunifu huo na usiwe wa kunakili ubunifu wowote kutoka ndani au nje ya nchi.
  • Uwasilishaji: Nembo inapaswa kuwasilishwa katika faili za “format” ya PDF, PNG, na JPEG.
  • Lugha: Maneno yote au alama yoyote itakayotumika inapaswa kuwasilishwa na tafsiri yake katika lugha ya Kiswahili na Kiengereza.

Angalizo

  • Ofisi ya Msajili wa Hazina itakuwa na haki ya kuisajili Nembo itakayoshinda kama alama yake ya huduma.
  • Uamuzi wa Jaji wa shindano hili ndio utakuwa uamuzi wa mwisho.
  • Mshindi wa shindano hilo atazawadiwa zawadi ya fedha taslim baada ya Manejimenti kuridhia na kuthibitisha na muhusika kuidhinisha juu ya matumizi ya Nembo.

Kila Mbunifu atapaswa kutuma Nembo yake pamoja na barua ya kuwasilisha Nembo hiyo kwa Msajili wa Hazina ikionesha: Jina kamili, picha ya ukubwa wa passpoti ya muhusika, Nambari ya Simu pamoja na anuani ya makazi.

Nembo hiyo itumwe kupitia barua pepe ya alex.malanga@tro.go.tz kabla ya saa 11:00 jioni ya tarehe 28/02/2025.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *