SIFA za Kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa

SIFA za Kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa
SIFA za Kujiunga na Chuo cha Serikali za Mitaa
Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) kilichopo Dodoma ni taasisi ya elimu inayotoa mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ujuzi na maarifa katika usimamizi wa serikali za mitaa na maendeleo ya jamii.
Chuo hiki kinatoa kozi mbalimbali zinazolenga kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma na sekta binafsi.
Namna ya Kuomba Kujiunga na Masomo Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI)
Astashahada (NTA Level 4 – Basic Technician Certificate)
Sifa za Kujiunga na Masomo Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI)
Sifa za kujiunga na kozi mbalimbali katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo zinatofautiana kulingana na ngazi ya kozi.
Ngazi ya Cheti (NTA Level 4)
Sifa za Kujiunga: Kidato cha Nne (Form Four) na ufaulu wa angalau daraja la nne (Division IV).
Ngazi ya Diploma (NTA Level 5)
Sifa za Kujiunga: Mwombaji awe amepata angalau ufaulu wa “Principal Pass” moja na “Subsidiary” katika mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) AU awe na Astashahada (NTA Level 4 Basic Technician Certificate) toka Chuo chochote kilichosajiliwa na kinachombulika na Serikali.
Pia awe amepata angalau ufaulu wa “D” 4 za Kidato cha Nne(CSEE). Masomo ya Dini hayahusiki.
Ngazi ya Diploma ya Juu (NTA Level 6)
Sifa za Kujiunga: Kidato cha Nne (Form Four) na ufaulu wa angalau daraja la nne (Division IV) na diploma ya NTA Level 5 katika kozi husika.
Kama mwombaji amefanya mtihani wa kidato cha nne zaidi ya mara moja, aambatanishe nakala za vyeti vyake vya awamu zote za mithani aliyofanya.
- Chuoni, Hombolo
- Kampasi ya Dodoma Mjini (Area C)
- Katika tovuti ya Chuo www.lgti.ac.tz
- Wizarani Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Library)
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
