SIFA Za Mwalimu wa Kujitolea

Filed in Elimu by on May 4, 2025 0 Comments
     
SIFA Za Mwalimu wa Kujitolea

SIFA Za Mwalimu wa Kujitolea

SIFA Za Mwalimu wa Kujitolea

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mwalimu wa kujitolea katika Shule za Elimu ya awali, Msingi, Sekondari, na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi anahitajika kuwa na sifa zifuatazo;

  • Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 18.
  • Awe Mhitimu aliyefaulu mafunzo ya Ualimu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Awe Mmiliki wa vyeti halisi vya kitaaluma na kitaalam.
  • Awe na Wadhamini wawili ambao ni watumishi wa Umma au viongozi wa Serikali za Mitaa/Kata au Viongozi wa dini.
  • Awe hajawahi kuhukumiwa kwa makosa ya kijinai au kuwa na kesi ya jinai.
  • Awe na tabia na mienendo inayokubalika na jamii.

Utaratibu wa Kupata Walimu wa Kujitolea ni kama ifuatavyo:

  • Kamati za shule/Vyuo kubainisha mahitaji halisi ya walimu.
  • Kipaumbele kitolewe kwa Waombaji waliojishughulisha na Shule/Chuo husika awali.
  • Waombaji kutoka maeneo yanayozunguka Shule/Chuo.
  • Kuweka matangazo kwenye
    Mbao za matangazo za Halmashauri, Kata, Shule, na Vyuo.
  • Vyombo vya habari kama Redio, Mitandao ya Kijamii, na Runinga.

Waombaji kuwasilisha Maombi kwa, Mkurugenzi wa Halmashauri au Mkuu wa Chuo, ikiwa na anuani kamili na mawasiliano (namba za simu/barua pepe).

Uchambuzi wa Maombi, Kamati za Shule/Vyuo kushiriki kikamilifu kuchambua maombi.

Orodha ya walimu waliochaguliwa kutangazwa kwenye mbao za matangazo na vyombo vya habari.

Walimu waliochaguliwa kujulishwa kwa barua.

Barua za Uteuzi zinaweza kufutwa kabla ya kusaini Mikataba ikiwa Serikali itaona ni lazima.

Unaweza Kusoma Mwongozo wa Walimu wa Kujitolea hapa.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *