SIMBA Kuifuata Al Masry 28 Machi 2025

SIMBA Kuifuata Al Masry 28 Machi 2025
SIMBA Kuifuata Al Masry 28 Machi 2025
Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam Alfajiri ya Alhamis March 28 kuelekea nchini Misri Kwaajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza robo Fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup 2024/2025 dhidi ya Al Masry utakaopigwa April 02,2025 katika uwanja wa Suez nchini humo.
Akizungumza katika Mkutano na wanahabari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa baadhi ya wachezaji ambao walikuwa katika timu ya Taifa ya Tanzania, wataunganisha moja kwa moja Misri
Ahmed amesema wanatambua mchezo dhidi ya Al Masry utakuwa mgumu lakini safari hii wamejipanga na lengo ni kuvuka hatua ya Robo Fainali.
“Kikosi kitaondoka nchini alfajiri ya tarehe 28 kuelekea Misri kwa kutumia ndege ya Egypt Air. Wachezaji wetu waliokuwa Taifa Stars wataungana na timu nchini Misri. Camara na Mukwala tayari wamewasili nchini kujiunga na wachezaji wenzao kwa ajili ya maandalizi ya safari”
“Kila Mwanasimba atambue kwamba pamoja na mipango tuliyonayo lakini lazima tujipange, lazima tujiandae na hasa kama timu yenyewe inatokea Misri. Ukiangalia michuano ya Afrika ilivyo utaona kwamba Misri ndio nchi iliyoingiza timu nne kwenye robo fainali”
“Tunakwenda kucheza na Al Masry tukijua tunakwenda kucheza mechi ngumu kwelikweli lakini dhamira tuliyojiwekea ni kufuzu nusu fainali,” alisema Ahmed
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
