Simba vs Azam FC kupigwa Benjamin Mkapa Stadium 24 February 2025

Simba vs Azam FC kupigwa Benjamin Mkapa Stadium 24 February 2025
Simba vs Azam FC kupigwa Benjamin Mkapa Stadium 24 February 2025
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imebadili uwanja na muda wa kuanza kwa mchezo namba 167 wa Ligi Kuu ya NBC (Simba SC vs Azam FC) ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa KMC Complex February 24, 2025 kuanzia saa 10:00 alasiri.
Mchezo huo sasa utafanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku Februari 24, 2025.
Sababu ya mabadiliko hayo ni kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo ambao ni moja ya michezo mikubwa ya Ligi Kuu ya NBC inayovuta hisia za watu wengi.
Uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 umekuwa ukitumika kwa michezo mingi mikubwa na inayohusisha mashabiki wengi zaidi.
Klabu shiriki (Simba na Azam) pamoja na wadau wengine wa mchezo huo wametumiwa taarifa rasmi ya mabadiliko haya na maandalizi yake yanaendelea vizuri yakiwemo mazingatio ya kiusalama.
Bodi inawatakia wadau wote maandalizi mema ya mchezo huo maarufu kwa jina la ‘Mzizima Derby’.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Simba vs Azam FC kupigwa Benjamin Mkapa Stadium 24 February 2025