SIMBA vs RS Berkane Kupigwa New Amaan Complex Zanzibar 25 May 2025

SIMBA vs RS Berkane Kupigwa New Amaan Complex 25 May 2025
SIMBA vs RS Berkane Kupigwa New Amaan Complex 25 May 2025
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limeuondoa mchezo wa Fainali ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba na RS Bekrane Katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.
Taarifa ambayo inadaiwa Simba imeshaipokea ni kwamba CAF imeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuanza kuhamisha maandalizi yote ya Fainali hiyo ya pili kwenye Uwanja wa Mkapa na sasa yahamie kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Taarifa hiyo, imekuwa ni kama pigo kubwa kwa Simba ambayo ina rekodi kubwa ya ushindi kwenye Uwanja wa Mkapa kwani mara ya mwisho kupoteza uwanjani hapo ni Machi 29 mwaka jana dhidi ya Al Alhy ya Misri ikipoteza Kwa bao 1-0 katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hata hivyo, Simba na TFF bado zinaendelea kupambana kubadilisha maamuzi hayo ya CAF kwa maombi maalumu juu ya mechi hiyo ya kihistoria, huku Simba ikisema kuwa taarifa ya uwanja utakaotumika itatolewa baada ya mchezo wa awali utakaochezwa Jumamosi tarehe 17, 2025.
Aidha, kwa taarifa kuhusu timu ya Berkane, inaelezwa tayari wameshapata sehemu ya kufikia Zanzibar kabla ya taarifa ya CAF.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: SIMBA vs RS Berkane Kupigwa Amaan Complex Zanzibar 25 May 2025, SIMBA vs RS Berkane Kupigwa New Amaan Complex Zanzibar 25 May 2025