SIMBA Yatinga Nusu Fainali CAF Confederation Cup 2024/2025

SIMBA Yatinga Nusu Fainali CAF Confederation Cup 2024/2025
SIMBA Yatinga Nusu Fainali CAF Confederation Cup 2024/2025
Klabu ya Simba SC imefanikiwa Kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF baada ya ushindi wa mikwaju ya penati 4-1.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kushuhudia Simba ikishinda 2-0 ndani ya dakika 90 na kusawazisha matokeo kwa ujumla (aggregate) kuwa 2-2 Kutokana na Kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Al Masry katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa nchini Misri.
Mabao ya Simba Katika mchezo huo yalifungwa na Elie Mpanzu dakika ya 22 na Steven Mkwala dakika ya 32.
Katika Mikwaju ya Penati, golikipa Moussa Camara ndiye aliyeibuka shujaa wa Simba kwa kuokoa mikwaju miwili ya Al Masry.
Naye Shomari Kapombe akafunga penati ya nne na kuihakikishia Simba tiketi ya Nusu Fainali ya CAF Confederation Cup 2024/2025.
Katika hatua ya Nusu Fainali Simba atakutana na Mshindi wa mchezo Katika ya Zamalek ya Misri dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: SIMBA Yatinga Nusu Fainali CAF Confederation Cup 2024/2025