Taarifa Kuhusu Mwenendo wa Ugonjwa wa Marburg Biharamulo, Kagera

Taarifa Kuhusu Mwenendo wa Ugonjwa wa Marburg Biharamulo, Kagera
Taarifa Kuhusu Mwenendo wa Ugonjwa wa Marburg Biharamulo, Kagera
Mnamo tarehe 20 Januari 2025, Serikali ilitoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Virusi vya Marburg (MVD) Mkoani Kagera ambapo idadi ya wagonjwa waliothibitishwa ni wawili (2) ambao walikwishafariki.
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau, wameendelea kufanya ufuatiliaji wa kina kwa watu wenye viashiria vya ugonjwa kwenye jamii na vituo vya kutolea huduma za afya ambapo wahisiwa 93 wenye dalili zinazofanana na ugonjwa wa Marburg walipimwa
kwa kuzingatia taratibu na kanuni za Afya ya kimataifa na kuthibitika kuwa hawana virusi vya Marburg.
Kwa mujibu wa taratibu za udhibiti wa magonjwa za kimataifa, wale wote waliotangamana na wagonjwa waliwekwa mahali maalum na kufuatiliwa kwa kipindi cha siku 21, na wamethibitika kutokuwa na maambukizi na sasa wameruhusiwa na wanaendelea na shughuli zao za kawaida.
Serikali inaendelea na mikakati ya kudhibiti ugonjwa huu ambapo mgonjwa wa mwisho kugundulika ilikuwa tarahe 28 January, 2025, hadi sasa siku 23 zimepita bila uwepo wa mgonjwa aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa Marburg wala kifo.
Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Afya inaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya dalili, madhara, pamoja na njia za kujikinga na ugonjwa huu.
Hata hivyo, katika kuongeza udhibiti dhidi ya magonjwa ya mlipuko, Wizara inaendelea kuwakumbusha kuwa, nchi yetu inaendelea kukabiliwa na tishio la magonjwa mengine yakiwemo ugonjwa wa Ebola na Homa ya Nyani (Monkeypox) yanayoendelea katika nchi mbalimbali Duniani.
Magonjwa hayo huambukizwa na kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kugusana na majimaji yaliyotoka kwa mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya ugonjwa husika.
Wizara inawakumbusha wananchi kuendelea kuchukua hatua zifuatazo;
- Kuwahi katika Vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya
uchunguzi na matibabu iwapo utakuwa na dalili za homa, uchovu wa mwili, kutapika au kuharisha damu au kutoka damu maeneo mbalimbali ya mwili. - Kutoa taarifa kwa haraka kwenye kituo cha kutolea huduma kilicho
karibu au kupiga simu namba 199 bila malipo endapo utamuona mtu
mwenye dalili hizo. - Kuepuka kumgusa mgonjwa au majimaji ya mwili bila kinga mfano
mate, machozi, damu, mkojo na kinyesi yatokayo kwa mgonjwa au mtu yeyote mwenye dalili zilizotajwa hapo juu. - Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono na epuka kusalimiana kwa kushikana mikono.
Kwa kuchukuwa hatua hizi na kuzingatia ushauri wa wataalamu, tunaweza kujikinga dhidi ya Marburg, Ebola, na Monkeypox.
Hali kadhalika Wizara inawakumbusha wananchi kuchukua tahadhari dhidi
ya ugonjwa wa Kipindupindu, ambao umeendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo nchini.
Ugonjwa huu kwa sehemu kubwa unadhibitiwa kwa kuzingatia kanuzi za afya na usafi wa mazingira kwa kutumia maji safi na salama, kuepuka kula matunda bila kusafisha, kula chakula cha moto na kuimarisha usafi wa mazingira na matumizi sahihi ya vyoo.
Wizara inatoa rai kwa wataalam wa Afya katika ngazi zote nchini, kuimarisha uchunguzi wa awali wa dalili za magonjwa haya katika vituo vyote vya kutolea huduma na kuimarisha zaidi utoaji wa elimu kwa umma juu ya namna ya kujikinga, kutambua na kubaini wahisiwa wa magonjwa
haya katika jamii.
Aidha, inaatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano na kuzingatia kanuni za afya za kinga na udhibiti kadribzinavyotolewa kupitia matangazo na njia zingine.
Wizara ya Afya inawashukuru watumishi wote wa afya walioko mstari wa mbele wakiwemo wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa moyo wa uzalendo na kujitoa kwao katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, ikiwemo ugonjwa wa virusi vya Marburg.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Kagera, Taarifa Kuhusu Mwenendo wa Ugonjwa wa Marburg Biharamulo