TAARIFA Mpya Kuhusu Ajira Za Uhamiaji

Filed in Ajira by on April 2, 2025 0 Comments
     
TAARIFA Mpya Kuhusu Ajira Za Uhamiaji

TAARIFA Mpya Kuhusu Ajira Za Uhamiaji

TAARIFA Mpya Kuhusu Ajira Za Uhamiaji

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Hivi karibuni Idara ya Uhamiaji ilitoa tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya Uhamiaji vijana wa Kitanzania kupitia tovuti na mitandao yake ya kijamii (Instagram, Twitter, Facebook).

Kufuatia tangazo hilo, kumekuwepo na Matapeli wanao walaghai Wananchi kupitia mitandao ya kijamii na baadhi yao kuwapigia simu au kuwatumia ujumbe kwa njia ya sms kwamba kuna nafasi za ajira na kuwataka kutuma fedha ili wawasaidie kupata nafasi hizo za ajira.

Idara ya Uhamiaji inapenda kuufahamisha Umma kuwa mchakato huo wa ajira ulishakamilika na uliendeshwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za ajira kama ilivyoainishwa kwenye tangazo la ajira.

Hivyo, Wananchi wanaombwa kupuuza na kutoa taarifa kwa vyombo vya
usalama pindi wanapopigiwa simu au kutumiwa ujumbe huo.

Taarifa rasmi za Idara kuhusu ajira na nyinginezo, hutolewa kupitia mifumo rasmi ya mawasiliano ikiwemo Vyombo vya Habari, tovuti ya Idara ambayo ni www.immigration.go.tz na mitandao yake ya kijamii (@UhamiajiTz).

Aidha, Idara ya Uhamiaji inaendelea na uchunguzi kwa lengo la kuwabaini wanaohusika na uhalifu huo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *