TAARIFA Mpya Kuhusu Ajira Za Zimamoto na Uokoaji

TAARIFA Mpya Kuhusu Ajira Za Zimamoto na Uokoaji
TAARIFA Mpya Kuhusu Ajira Za Zimamoto na Uokoaji
Hivi karibuni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilitoa Tangazo la Ajira na Kuitwa kwenye usaili vijana wa kitanzania kupitia tovuti, Magazeti na Mitandao ya Kijamii (Instagram, X- twitter na Facebook).
Kufuatia matangazo hayo, kumekuwapo na Watu wasio waaminifu, wenye nia ovu na wapotoshaji (Matapeli) wanao walaghai Wananchi kwa kuwapigia simu au kuwatumia ujumbe kwa njia ya simu (SMS) na baadhi yao kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna fomu za ajira na kuwataka kutuma fedha ili wawasaidie kupata nafasi hizo za ajira.
Taarifa hizo hazina ukweli na wananchi wanaombwa kuzipuuza pamoja na kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama pindi wanapopigiwa simu au kutumiwa ujumbe wa aina yoyote wenye viashiria vya utapeli.
Aidha, wananchi wanajulishwa kuwa taarifa rasmi kuhusu ajira na nyinginezo, hutolewa kupitia mifumo rasmi ya mawasiliano ikiwemo vyombo vya habari, tovuti ambayo ni www.zimamoto.go.tz na akaunti rasmi za mitandao ya kijamii zinazojulikana kwa jina la (zimamototanzania).
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama linaendelea na uchunguzi kwa lengo la kuwabaini wanaohusika na upotoshaji huo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria “Zimamoto na Uokoaji, Okoa Maisha na Mali Piga 114”

TAARIFA Mpya Kuhusu Ajira Za Zimamoto na Uokoaji
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Awo wenyewe walisem Kam umechaguluwa utatumiwa message