TAARIFA Mpya Kuhusu Matokeo ya Usaili wa Kuandika Ajira za TRA 2025

TAARIFA Mpya Kuhusu Matokeo ya Usaili wa Kuandika Ajira za TRA 2025
TAARIFA Mpya Kuhusu Matokeo ya Usaili wa Kuandika Ajira za TRA 2025, Matokeo ya Usaili Ajira za TRA 2025.
Mamlaka ya Mapato Tanzania ilitangaza nafasi za kazi kuanzia tarehe 6 hadi 19 Februari, 2025, ambapo tarehe 21 Machi, 2025 Mamlaka ilitoa taarifa kwa umma kwamba baada ya kufunga zoezi la kupokea jumla ya maombi 135,027 yalipokelewa.
Kati ya maombi hayo, maombi 112,952 yalikidhi vigezo vya kuitwa kwenye usaili wa kuandika na tarehe 23 Machi, 2025 Mamlaka ilitoa fursa ya siku mbili (24 na 25 Machi, 2025) kwa waomba kazi ambao walidhani walistahili kuitwa kwenye usaili wa kuandika ila hawakuitwa na baada ya kutolewa kwa fursa hiyo jumla ya maombi 71 yalikidhi vigezo na hivyo kufanya jumla ya maombi 113,023 kukidhi vigezo vya kufanya usaili wa kuandika.
Mamlaka imetoa taarifa kuwa, katika maombi hayo, wapo waombaji walioomba nafasi zaidi ya moja, ambapo maombi 113,023 yaliyokidhi vigezo vya kufanya usaili wa kuandika yaliombwa na waomba kazi 86,314.
Kati yao, waombaji waliofanya usaili wa kuandika walikuwa 78,544 ambao ni sawa na asilimia 91, waombaji 7,770 ambao ni sawa na asilimia 9 hawakushiriki kwenye usaili kutokana na sababu mbalimbali.
Kama tulivyowataarifu hapo awali kuwa zoezi hili la usaili linafanywa na Mshauri Elekezi ambaye ni Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
Mshauri huyu alipatikana kupitia mchakato wa manunuzi kufuatia historia na uzoefu wake katika kuendesha masuala ya mitihani kwa weledi na uadilifu.
Hivyo NBAA wanaendesha zoezi la usaili katika hatua zote mpaka waajiriwa watakapopatikana.
Mamlaka ya Mapato Tanzania haihusiki na kutunga, kuratibu na kusahihisha mitihani ya usaili huo, hivyo itaendelea kubaki kama Msimamizi wa zoezi hilo tu.
Kutokana na mpango kazi uliopitishwa, matokeo ya usaili wa maandishi yanatarajiwa kuwasilishwa na Mshauri Elekezi (NBAA) tarehe 23 Aprili, 2025 na yatatangazwa tarehe 26 Aprili, 2025 kupitia tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Usaili wa vitendo kwa nafasi za Madereva na Waandishi Waendesha Ofisi unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 2 hadi 4 Mei, 2025 ambao utafuatiwa na usaili wa mahojiano unaotegemea kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 7 hadi 9 Mei, 2025.
Baada ya Mshauri Elekezi kuwasilisha matokeo ya usaili wa mahojiano watakaofanikiwa kushinda usaili huo wataarifiwa tarehe 18 Mei, 2025 na watatakiwa kuanza mafunzo elekezi tarehe 22 Mei, 2025 hadi Tarehe 2 Juni, 2025 ambapo wataajiriwa na kuanza kazi rasmi.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: TAARIFA Mpya Kuhusu Matokeo ya Usaili wa Kuandika Ajira za TRA 2025
Natafuta ajira
Natafta kazi
Mimi mbona nimetuma maombi na nimezingatia hatua zote lakini nimekosa na sijalewa taarifa yeyote ile
NATAFUTA KAZI
26
Natafuta kazii
Natafuta kazi