TAARIFA Mpya Kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuhusu Wazimamoto wa Kujitolea

Filed in Ajira by on May 19, 2025 0 Comments
     
TAARIFA Mpya Kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuhusu Wazimamoto wa Kujitolea

TAARIFA Mpya Kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuhusu Wazimamoto wa Kujitolea

TAARIFA Mpya Kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuhusu Wazimamoto wa Kujitolea

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA EPUKA MATAPELI NA UPOTOSHAJI KUHUSU WAZIMAMOTO WA KUJITOLEA

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma tarehe 15 Mei, 2025 lilitoa Tangazo la kuwapata vijana wa kujitolea ili waweze kujiunga na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Dodoma.

Kufuatia Tangazo hilo, kumekuwapo na watu wasio waaminifu, wenye nia ovu na wapotoshaji (Matapeli) wanao walaghai Wananchi kwa kuongeza tangazo kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna malipo watapata utakapokuwa mzima moto wa kujitolea na wameainisha viwango vya malipo hayo.

Taarifa hizo hazina ukweli na wananchi wanaombwa kuzipuuzia pamoja na kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama pindi wanapopigiwa simu au kutumiwa ujumbe wa aina yoyote wenye viashiria vya utapeli.

Wananchi wanajulishwa kuwa taarifa rasmi kuhusu Wazimamoto wa Kujitolea au nyinginezo, hutolewa kupitia mifumo rasmi ya mawasiliano ikiwemo vyombo vya habari, tovuti ambayo ni www.zimamoto.go.tz na akaunti rasmi za mitandao ya kijamii zinazojulikana kwa jina la (zimamototanzania)

Aidha, ikumbukwe kuwa, Wazimamoto wa Kujitolea hawalipwi. Hii ni nafasi ya uzalendo na kutoa huduma kwa jamii, si ajira ya malipo. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wote wanaopotosha jamii kwaajili ya kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Zimamoto na Uokoaji, Okoa Maisha na Mali Piga 114”

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!