TANZIA Papa Francis Afariki Dunia

Filed in Habari by on April 21, 2025 1 Comment
     
TANZIA Papa Francis Afariki Dunia

TANZIA Papa Francis Afariki Dunia

TANZIA Papa Francis Afariki Dunia

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Papa Francis amefariki Dunia Leo Jumatatu ya Pasaka tarehe 21 April 2025, akiwa na umri wa miaka 88 katika makazi yake, Casa Santa Marta, Vatican.

Muda mfupi uliopita, Mwadhama, Kardinali Farrell, alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis, kwa maneno haya:

“Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa sina budi kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko”.

Papa huyo raia wa Argentina ametumia wiki tano katika hospitali akipambana na nimonia.

Papa Francis alihudumu kama Papa kwa takriban miaka 12, baada ya kuchaguliwa kwake tarehe Machine 13, 2013 kufuatia kujiuzulu kwa mshtuko kwa mtangulizi wake Benedict XVI.

Papa huyo, ambaye sehemu ya pafu moja ilitolewa akiwa na umri wa miaka 20 na alikuwa amepambana na matatizo ya afya kwa miaka mingi, alilazwa Gemelli tarehe 14 February.

Katika miaka ya hivi majuzi alilazwa hospitalini mara kadhaa katika Gemelli ambapo alitibiwa katika chumba cha orofa ya 10 kilichohifadhiwa mapapa pekee.

Kifo cha papa kinakuja wakati wa Mwaka wa Yubile wa Vatikani, tukio Kuu la kidini linalofanyika Roma kila robo karne.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Sixmund ndabita says:

    Ndio nataka kujiungas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *