TFF yavifungia Viwanja Vitatu Kwa kukosa Vigezo

Filed in Michezo by on March 10, 2025 0 Comments
     
TFF yavifungia Viwanja Vitatu Kwa kukosa Vigezo

TFF yavifungia Viwanja Vitatu Kwa kukosa Vigezo

TFF yavifungia Viwanja Vitatu Kwa kukosa Vigezo

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuvifungia viwanja vitatu kutumika kwa michezo ya ligi kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na kisheria vinavyotakiwa kutumika kwa Ligi Kuu.

Viwanja vilivyokumbana na rungu hilo ni Jamhuri (Dodoma), CCM Kirumba (Mwanza) na Liti (Singida).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Machi 10, 2025, na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo imesema kuwa miundombinu ya viwanja hivyo haikidhi masharti yaliyowekwa katika Kanuni ya Leseni za Klabu.

Hivyo, timu zinazotumia viwanja hivyo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia viwanja vingine vinavyokidhi vigezo hadi marekebisho yatakapofanywa na TFF kufanya ukaguzi upya.

TFF imezikumbusha klabu zote kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vyake ili kuhakikisha michezo inachezwa katika mazingira salama na yanayokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!