UFAFANUZI Penati ya JKU iliyokataliwa vs Singida Black Stars

Filed in Michezo by on April 26, 2025 0 Comments
     
UFAFANUZI Penati ya JKU iliyokataliwa vs Singida Black Stars

UFAFANUZI Penati ya JKU iliyokataliwa vs Singida Black Stars

UFAFANUZI Penati ya JKU iliyokataliwa vs Singida Black Stars

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Abubakary Nizar, kijana kutoka akademi ya Azam FC anayechezea JKU kwa mkopo, amekuwa mtanzania wa kwanza kuhukumiwa kwa sheria iliyotungwa kwa sababu ya Kiungo Mshambuliaji wa Brazil, Neymar Jr.

Akipiga penati ya tatu ya timu yake dhidi ya Singida Black Stars kwenye mechi ya kwanza ya Kombe la Muungano 2025, Nizar alisita na kusikilizia kwanza akiwa katika hatua ya mwisho kabla ya kuugusa mpira.

Sheria ya upigaji penati inamkataza mpiga penati kufanya hivyo, kwani anatakiwa anapoufikia mpira aupige moja kwa moja bila kusikilizia kwanza.

Kama anataka kusita na kusikilizia kwanza basi afanye hivyo kabla ya kuufikia mpira, yaani kabla ya hatua ya mwisho.

Sheria hii ilitungwa na Bodi ya Kimataifa ya sheria za Soka, IFAB, mwaka 2010 kwaajili ya kumdhibiti nyota chipukizi wa klabu ya Santos ya Brazil, Neymar Jr.

IFAB ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kutunga, kubadilisha au kurekebisha sheria za soka, kisha huwapa FIFA wazitumie.

Nenymar wakati huo akiwa chini ya miaka 17, alikuwa amelitawala soka la Brazil akiwatesa wapinzani kwa kila aina ya ujanja na maarifa.

Katika moja ya mambo aliyowatesa nayo ni aina hii ya upigaji wake wa penati.

Hukumu ya kosa hili ni penati kuhesabiwa imepotea, sio kurudiwa na mpigaji kuoneshwa kadi ya njano.

Na hiki ndicho kilichomkuta kijana Abubakary Nizar wa JKU SC April 24,2025 kwenye mchezo wa Kwanza wa Kombe la Muungano dhidi ya Singida Black Stars.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *