Uwanja wa Kimataifa Kujengwa Dodoma

Uwanja wa Kimataifa Kujengwa Dodoma
Uwanja wa Kimataifa Kujengwa Dodoma, Dodoma Stadium yajengwa
Uwanja unaobeba watu 32000 Kujengwa Dodoma, Sh350 bilioni Kujenga Uwanja wa Kimataifa wa Dodoma.
Serikali ya Tanzania tayari imesaini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa mchezo wa mpira wa miguu Jijini Dodoma na mkandarasi kampuni ya LimontaI Spa ya nchini Italy wenye thamani ya zaidi ya Sh350 bilioni.
Mradi huo utatekelezwa kwa miaka miwili kuanzia sasa, huku ukitarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji zaidi ya 32,000 ambao ni mradi wa pili wa ujenzi wa viwanja vipya vilivyotangazwa na Serikali.
Profesa Kabudi alisema kuwa mradi huo ni kielelezo cha kuendelea kuimarisha sekta ya michezo nchini.
Kusainiwa kwa mkataba huo kunaondoa sintofahamu ya muda mrefu ya ujenzi wa uwanja Dodoma kutokana na kukwama kwa ufadhili wa Serikali ya Morocco ambapo kwa sasa mradi huo utafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Jobs application