VIINGILIO Simba vs Al Masry 09 April 2025

Filed in Michezo by on March 26, 2025 0 Comments
     
VIINGILIO Simba vs Al Masry 09 April 2025

VIINGILIO Simba vs Al Masry 09 April 2025

VIINGILIO Simba vs Al Masry 09 April 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amewahakikishia Wanasimba kuwa mchezo wa mkondo wa pili robo Fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry utapigwa April 09,2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ahmed amesema kuwa maafisa wa CAF wamefanya ukaguzi wa uwanja huo na wameridhishwa na maboresho yaliyofanyika licha ya kuwa bado hawajatoa majibu

Kuelekea mchezo huo muhimu kwa Simba kuwania Kufuzu Nusu Fainali ya Michuano hiyo Ahmed ametangaza viingilio ambapo Mzunguko itakuwa Tsh 5,000.

Viingilio vingine vya mchezo wa Simba dhidi ya Al Masry April 09,2025 ni Tsh 10,000 Kwa Viti vya Orange, Tsh 15,000 Kwa VIP C, Tsh 30,000 Kwa Vip B, Tsh 40,000 kwa VIP A, Tsh 150,000 Kwa  Platinum huku Tanzanite ikiwa Tsh 250,000.

Aidha Tiketi zimeanza kuuzwa Kuanzia Sasa.

Ahmed amesema kuwa kwenye mechi hii wanataka kuingiza mashabiki kati ya 50,000 hadi 60,000 hivyo wanafafanya hamasa kubwa, mtaa kwa mtaa na matawi yote ili kuwahamasisha Wanasimba kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo muhimu.

Ahmed ameongeza kuwa Safari hii wamekuja na tukio la kipekee kabisa. Wamendaa Bonanza ambalo litahusisha wafanyakazi wa benki ambao ni mashabiki wa Simba. Tukio hili litahusisha benki zote ambazo zitathibitisha kushiriki. Sharti ni moja washiriki ambao watacheza wawe mashabiki wa Simba.

“Bonanza litafanyika kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 6 Aprili, 2025. Kutakuwa nazawadi mbalimbali kwa washindi likiwepo kombe,”alisema Ahmed

Pia Ahmed ametangaza kauli mbiu itakayotumika kwenye mchezo huo kuwa ni HII TUNAVUKA. Baada ya kucheza robo fainali ya mashindano ya CAF kwa misimu mitano mfululizo, safari hii Simba imepania kwenda nusu fainali

Katika hatua nyingine, Simba imetangaza kuwa mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi za mechi yao dhidi ya Constantine watazitumia kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Masry ya Misri.

Uamuzi huo umekuja baada ya CAF kuiadhibu Simba kwa kucheza mechi moja bila mashabiki na faini ya dola 40,000 kufuatia vurugu zilizoibuka kwenye mechi yao dhidi ya CS Sfaxien ya Algeria mnamo Desemba 15, 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *