VIINGILIO Vipya Simba vs RS Berkane 25 May 2025

VIINGILIO Vipya Simba vs RS Berkane 25 May 2025
VIINGILIO Vipya Simba vs RS Berkane 25 May 2025
Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa mashabiki 16,000 waliokuwa tayari wamenunua tiketi kwaajili ya mchezo wa Fainali ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa sasa tiketi zao zitatumika katika Tamasha la Simba Day 2025.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Ahmed Ally amesema kuwa Uwanja wa Amaan Zanzibar ambao mchezo huo utapigwa unaingiza mashabiki 15,000 pekee hivyo tayari kuna watu 10,000 ambao wasingekuwa na nafasi hivyo Klabu umeamua kuzitumia tiketi hizo kwenye Simba Day.
Ahmed ameongeza kuwa baada ya kuthibitika mchezo utapigwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar wamesitisha zoezi la kuuza tiketi na waliokuwa wamenunua wanatakiwa kuzitunza hadi itakapofika Simba Day.
Aidha Ahmed amesema kuwa baada ya kufunga zoezi hilo sasa tiketi zitaanza kuuzwa upya kwaajili ya Fainali itakayopigwa Amaan Zanzibar May 25, 2025.
Ahmed ametaja viingilio vya mchezo huo wa pili wa Fainali dhidi ya RS Berkane kuwa ni, Tsh 50,000 kwa VIP A, Tsh 30,000 kwa Jukwaa la Urusi huku
Mzunguko ikiwa ni Sh. 10,000 tu.
Aidha tiketi hizo tayari zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao.
Ahmed ameongeza kuwa kutakuwa na usafiri wa Ndege wa kwenda na kurudi siku hiyo hiyo ya mchezo ambapo gharama yake itakuwa Shilingi 350,000.
Pia Mashabiki watakaolipa kiasi hicho Simba itawapatia tiketi za VIP A, jezi za Fainali pamoja na usafiri wa kutoka na kurudi Uwanja wa Ndege.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: VIINGILIO Simba vs RS Berkane 25 May 2025, VIINGILIO Vipya Simba vs RS Berkane 25 May 2025