VITU Vya Kwenda Navyo Kwenye Usaili wa Mahojiano na Vitendo TRA 2025

Filed in Usaili by on April 28, 2025 0 Comments
     
VITU Vya Kwenda Navyo Kwenye Usaili wa Mahojiano na Vitendo TRA 2025

VITU Vya Kwenda Navyo Kwenye Usaili wa Mahojiano na Vitendo TRA 2025

VITU Vya Kwenda Navyo Kwenye Usaili wa Mahojiano na Vitendo TRA 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Usaili wa vitendo na Mahojiano (Practical and Oral Interviews) Ajira za TRA unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 02 Mei, 2025 hadi tarehe 14 Mei, 2025.

Usaili wa Vitendo utafanyika Kuanzia tarehe 2 hadi tarehe 4 May 2025, huku Usaili wa Mahojiano ukifanyika Kuanzia tarehe 12 hadi tarehe 14 May 2025.

Kuelekea usaili huo hivi hapa ni Vitu Vya lazima vya kwenda navyo ama Kuzingatia.

Kuhusu Vitambulisho: Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwaajili ya utambuzi.

Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na;

  • Kitambulisho cha Taifa.
  • Kitambulisho cha Mkaazi.
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura.
  • Leseni ya Udereva.
  • Hati ya kusafiria au Barua ya Utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa.

Vitambulisho tofauti na vilivyoorodheshwa hapo juu havitatambuliwa.

Kuhusu Vyeti: Wasailiwa Wote wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI (Original).

Vyeti vinavyotakiwa ni;

  • Kuanzia Cheti Cha Kuzaliwa.
  • Cheti Kidato cha IV, VI.
  • Stashahada.
  • Stashahada ya Juu.
  • Shahada na kuendelea Kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  • Wasailiwa watakaowasilisha

“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (Form IV and Form VI result slips) HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

Kuhusu Chakula, Usafiri na Malazi: Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.

Kuhusu muda wa Kufika: Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili kulingana na ratiba husika, Muda wa kufika ni Saa moja kamili asubuhi.

Kwa wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania: wao wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husíka (kama TCU, NACTVET au NÉCTA).

Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma: wao wanapaswa kwenda na vyeti vyao Halisi vya Usajili na Leseni za kufanyia kazi (kwa wanaohusika).

Aidha wasailiwa hawaruhusiwi kuja na simu, saa au kifaa chochote cha kielekroniki kwenye eneo la usaili.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!