Wafahamu Al Masry wapinzani wa Simba Robo Fainali CAF Confederation Cup 2024/25

Wafahamu Al Masry wapinzani wa Simba Robo Fainali CAF Confederation Cup 2024/25
Wafahamu Al Masry wapinzani wa Simba Robo Fainali CAF Confederation Cup 2024/25
Klabu ya Al Masry maarufu (Green Eagle) ilianzishwa tarehe 18 March 1920 ikiwa ni moja kati ya timu tano bora kwa taifa la Misri ambapo Simba itatakiwa kujiandaa kupambana nayo kwa umakini kutokana na ubora wa kikosi chao.
Hata hivyo haina mafanikio Katika michuano ya CAF na hata nyumbani ukilinganisha na Vilabu vingine vya Misri.
Mafanikio makubwa ya Al Masry katika mashindano ya klabu Afrika miaka ya hivi karibuni ni kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2018 baada ya kuitoa Simba raundi ya pili, ingawa pia imewahi kutinga hatua kama hiyo kwenye Kombe la CAF 2002.
Kwa msimu huu Al Masry ilikuwa Kundi D ukimaliza nafasi ya pili ikifunga mabao saba na kuruhusu manne ikikusanya jumla ya pointi tisa kwenye kundi lililoongozwa na Zamalek Wakiwa na pointi 14.
Kwenye mechi hizo sita za makundi, Al Masry ilishinda michezo miwili yote ya nyumbani dhidi ya Black Bulls ya Msumbiji (3-1) na Enyimba ya Nigeria (2-0), kisha ikatoa sare tatu na kupoteza mmoja dhidi ya Zamalek (1-0).
Kikosi hicho kinacho fundishwa na kocha mzawa Ali Maher mwenye umri wa miaka 51 kinatumia mifumo mitatu tofauti ambayo 4-3-2- 1, 4-1-4-1 na 4-3-3 ikitegemea na ubora wa wapinzani wao wanaokutana nao kwenye mashindano.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Wafahamu Al Masry wapinzani wa Simba Robo Fainali CAF Confederation Cup 2024/25