WALIOITWA Kwenye Usaili TAWA, Kuitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori

WALIOITWA Kwenye Usaili TAWA, Kuitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
WALIOITWA Kwenye Usaili TAWA, Kuitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa
kuendeshwa kuanzia tarehe 06-03-2025 hadi 08-03-2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka. - Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za
Mwombaji. - Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA) - Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika. - Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.
KUITWA KWENYE USAILI MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI (TAWA) 24-02-2025
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Kuitwa Kwenye Usaili Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori, WALIOITWA Kwenye Usaili TAWA