WAMISRI Kuamua Yanga vs Simba 25 June 2025

WAMISRI Kuamua Yanga vs Simba 25 June 2025
WAMISRI Kuamua Yanga vs Simba 25 June 2025
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza majina ya waamuzi watakaosimamia mchezo wa watani wa jadi, Yanga SC dhidi ya Simba SC, utakaopigwa Jumatano, Juni 25, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo namba 184 utaamuliwa na waamuzi kutoka Misri ambapo Mwamuzi wa kati ni Amin Mohamed Amin Omar (Misri), mwamuzi msaidizi wa kwanza Mahmoud Ahmed Abo El Regal (Misri), Mwamuzi Msaidizi wa pili Samir Gamal Saad Mohamed (Misri), Mwamuzi wa akiba ni Ahmed Mahrous Elghandour (Misri).
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa ni Salim Omary Singano (Tanga, Tanzania) na Mkaguzi wa waamuzi ni Alli Mohamed (Somalia).
Mchezo huo utapigwa Kuanzia Saa 11:00 Jioni.
Ikumbukwe kuwa Yanga inaongoza Ligi Kwa alama 79 tofauti ya alama moja dhidi ya Simba SC wenye alama 78, hivo mchezo huo wa kiporo ndio utaamua Bingwa wa NBC 2024/2025.

WAMISRI Kuamua Yanga vs Simba 25 June 2025
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
