WANAFUNZI 1413 wa Diploma Wapata Mikopo Dirisha la Machi 2025

WANAFUNZI 1413 wa Diploma Wapata Mikopo Dirisha la Machi 2025
WANAFUNZI 1413 wa Diploma Wapata Mikopo Dirisha la Machi 2025
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu HESLB inawatangazia wanafunzi wote walioomba mikopo na umma kwa ujumla kuwa jumla ya wanafunzi 1,413 walioomba mikopo dirisha la mwezi Machi, 2025, wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 3,388,017,500.00 hadi kufikia Ijumaa, tarehe 16 Mei, 2025.
Idadi hiyo, ni ongezeko la wanafunzi 540 kutoka wanafunzi 873 ambao tulitangaza kuwapangia mikopo yenye thamani ya TZS 1,944,922,500.00 katika taarifa iliyoitangazwa tarehe 5 Mei, 2025.
Katika mwaka huu wa masomo 2024/2025, jumla ya wanafunzi 9,144 wa Stashahada wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 23,981,542,101.00 kati yao; wanafunzi wa mwaka wa kwanza ni 7,040 wenye mikopo ya jumla ya TZS 18,242,010,001.00 na wanafunzi wanaoendelea ni 2,104 wenye mikopo ya thamani ya TZS 5,739,532,100.00.
Kupitia taarifa hii, upangaji wa mikopo kwa mwaka 2024/2025 umekamilika kwa wanafunzi wa stashahada.
Kuangalia Kama Umepata Mkopo Bonyeza Hapa
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: WANAFUNZI 1413 wa Diploma Wapata Mikopo Dirisha la Machi 2025