Wanamichezo 10 Bora Wanaolipwa Pesa nyingi zaidi 2025

Wanamichezo 10 Bora Wanaolipwa Pesa nyingi zaidi 2025
Wanamichezo 10 Bora Wanaolipwa Pesa nyingi zaidi 2025
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameongoza orodha ya Forbes ya wanamichezo wanaolipwa fedha nyingi zaidi kwa mwaka wa tatu mfululizo, huku nyota wa NBA Stephen Curry akipanda hadi nafasi ya pili.
Jarida la forbes limesema kuwa Ronaldo, ambaye ameongoza orodha hiyo mara tano wakati wa uchezaji wake, na ameongeza mapato yake yote kwa $15m hadi $275m (takriban £206m).
Idadi hiyo imezidiwa tu na bondia bingwa wa zamani wa Dunia Floyd Mayweather, ambaye alipata $300m mwaka 2015 (wakati huo £194m) na $275m mwaka 2018 ( £205m).
Ronaldo mwenye umri wa miaka 40, alihamia kwenye Ligi ya Saudi Pro League Katika Klabu yaAl Nassr December 2022 na amejipatia mapato makubwa kupitia uidhinishaji nje ya uwanja na mikataba ya udhamini inayoungwa mkono na wafuasi wake wa mitandao ya kijamii, ambao kwa sasa wanafikia milioni 939.
Mlinzi wa Golden State Warriors Curry, ambaye alikua mchezaji wa kwanza wa NBA kufikisha pointi 4,000 katika taaluma yake mwezi March, alipanda hadi wa pili baada ya kupata $156m (takriban £117m).
Bondia wa Uingereza Tyson Fury alipanda hadi wa tatu kwa $146m (takriban £109m) licha ya kupoteza mataji yake ya uzito wa juu kwa Oleksandr Usyk wa Ukraine mwezi December.
Mpinzani wa muda mrefu wa Ronaldo Lionel Messi amezidi kuwa nyuma ya Mreno huyo baada ya kushuka kutoka nafasi ya tatu hadi ya tano.
Wanamichezo 10 Bora wanaolipwa Pesa nyingi zaidi 2025
- Cristiano Ronaldo – Soka: $275m (£206.6m)
- Stephen Curry – Mpira wa vikapu: $156m (£117.2m)
- Tyson Fury – Ndondi: $146m (£109.7m)
- Dak Prescott, American football: $137m (£103m)
- Lionel Messi- Soka: $135m (£101.4m)
- LeBron James – Mpira wa vikapu: $133.8m (£105.5m)
- Juan Soto – baseball: $114m (£85.7m)
- Karim Benzema- Soka: $104m (£78.2m)
- Shohei Ohtani- baseball: $102.5m (£77m)
- Kevin Durant – Mpira wa vikapu: $101.4m (£76.2m)
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
