Washindi wa tuzo za Tanzania Comedy Awards 2024/2025

Filed in Habari by on February 23, 2025 0 Comments
     
Washindi wa tuzo za Tanzania Comedy Awards 2024/2025

Washindi wa tuzo za Tanzania Comedy Awards 2024/2025

Washindi wa tuzo za Tanzania Comedy Awards 2024/2025, Orodha ya Washindi wa tuzo tuzo za wachekeshaji 2024/2025.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Tuzo za wachekeshaji (Tanzania Comedy Awards 2024/2025) zimegawiwa February 22, 2025 Katika Ukumbi waThe Super Dome Masaki, Jijini Dar Es Salaam.

Mchekeshaji Dogo Sele ndiye aliyezifungua tuzo hizo kwa kushinda kipengele cha ‘Best Funny Kid’.

Hata hivyo katika tuzo hizo Coy Mzungu ambaye ni mchekeshaji na mwanzilishi wa jukwaa la vichekesho ‘Cheka Tu’ ametunukiwa Tuzo Maalumu ya ‘Game Changer’.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alimtangaza Conrad Kennedy Coy, ‘Coy Mzungu’ kuwa mshindi wa Tuzo Maalumu ya Game Changer katika tuzo za kwanza za Tanzania Comedy Awards 2025/2025.

Coy amepokea tuzo hiyo kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya vichekesho nchini. Hususani kupitia Cheka Tu ambayo imewapa jukwaa wasanii wengi wa vichekesho.

Mchekeshaji ‘Jol Master’ ameibuka mshindi wa tuzo ya Mchekeshaji Bora Maalum wa Mwaka, Katika kipengele hicho, Jol Master alikuwa akichuana na wachekeshaji wengine walioteuliwa, akiwemo Kipotoshi, Deo Matius na Nalim Noseph.

Mchekeshaji maarufu, Lucas Mhavile ‘Joti’ ameibuka mshindi wa tuzo ya Best Legend Peoples Choice of The Year.

Hii ni tuzo ya pili kwa Joti kushinda usiku huu wa tuzo, ambapo ya kwanza alishinda kama Best Comedian Actor of the Year.

Kwenye tuzo yake ya pili alikuwa akichuana na wachekeshaji wakongwe wengine wakiwemo Bambo, Asha Boko, Maufundi, Mukwele, Kigwedu, Senga, Muhogo Mchungu na Brother K.

Mchekeshaji Asma Jamida ameshinda tuzo ya Mchekeshaji Bora wa Kike katika tuzo hizo.

Mchekeshaji mwingine aliyeibuka kidedea kwenye tuzo hizo ni Nanga ambae ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wa kiume wa mwaka.

Tuzo ya Shoo bora ya kwenye Runinga imechukukiwa na Kitim Tim ambapo imeshinda kipengele hiyo, mbele ya Tv shoo zingine ambazo ni Futuhi, original comedy na mbambalive.

Neila Manga ashinda tuzo ya Best Female stand up comedian of the Year, pia, Neila Manga ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wima wa kike ambapo alikuwa akiwania pamoja na wachekeshaji wengine ambao ni Mambise na mama Mawigi.

Kwa upande wa Mc Eliud, Mr Sukari yeye ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wa wima ‘Best Stand Up Comedy’, tuzo ambayo alikuwa anawania pamoja na wachekeshaji wengine akiwemo Leornado, kipotoshi na Deo Rashid.

Mama Mawingi yeye ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wa kike wa kidijitali, Kwa upande wa wanaume ameshinda TX Dulla ambapo amewashinda Steve, Ndaro, Nanga.

Lakini pia Ndaro na Steve mweusi wameshinda tuzo ya Best Comedy Duo of the Year.

Hii ni tuzo ya ushirikiano kwenye ushekeshaji Wameshinda tuzo hiyo wakiwapiga chini Nanga na Shafii, Zuli Comedy.

Na Safina wa mizengwe ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa vichekesho wa kike.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere ameshinda tuzo ya kiongozi mchekeshaji Tanzania.

Katika kipengele hicho, Makongoro alikuwa anashindana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Richard Hananja na Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Aggrey Mwanri.

Mgeni Rasmi Katika tuzo hizo alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Orodha Kamili ya Washindi wa tuzo za Tanzania Comedy Awards 2024/2025

  1. Champion Of Comedy – Rais Samia Suluhu Hassan.
  2. Hall Of Fame – King Majuto.
  3. Tuzo ya heshima – Coy Mzungu.
  4. Best Comedian Actor Of The Year – Joti.
  5. Best Comedy Special Award – Jol Master.
  6. Best Male Comedian Of The Year – Nanga.
  7. Best Comedian Of The Year People’s Choice – Leonardo.
  8. Best Female Comedian Of The Year – Asma.
  9. Best Male Stand Up Comedian Of The Year – Eliud samwel.
  10. Best Female Stand Up Comedia Of The Year – Neila.
  11. Best Funny Leader Of The Year – Makongoro Nyerere.
  12. Legend People’s Choice – Joti.
  13. Best Comedy Tv Show – Kitimtim.
  14. Best Kid Comedian – Dogo Sele.
  15. The award for Tanzania’s Comedian Leader – Makongoro Nyerere.
  16. Aliyemchekesha zaidi Rais Sami-  Said Said.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *