Wawili wakutwa na Ugojwa wa Mpox Tanzania

Wawili wakutwa na Ugojwa wa Mpox Tanzania
Wawili wakutwa na Ugojwa wa Mpox Tanzania
Wizara ya Afya imethibitisha kesi mbili za ugonjwa wa Mpox nchini Tanzania baada ya uchunguzi wa maabara kufanyika kwa wahisiwa.
Kesi hizi zilipatikana kwa wagonjwa waliokuwa na dalili kama vile homa, vidonda kwenye ngozi, maumivu ya viungo, na vipele.
Serikali imesema kuwa inachukua hatua madhubuti kudhibiti maambukizi kwa kufuatilia wahisiwa wengine na kutoa elimu kwa umma juu ya njia za kujikinga.
Wananchi wanahimizwa kuepuka kugusana moja kwa moja na wagonjwa, kutumia vifaa binafsi, na kunawa mikono mara kwa mara.
Aidha, Wizara imetoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Marburg, ikieleza kuwa kwa siku 41 zilizopita hakuna mgonjwa mpya aliyeripotiwa, ikimaanisha kuwa udhibiti wa ugonjwa huu unaendelea vyema.
Wananchi wanashauriwa kuchukua tahadhari na kuripoti dalili zozote za Mpox kwa kupiga simu 199 bila malipo.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
