YANGA Mabingwa Wapya Kombe la Muungano 2025

Yanga Mabingwa Wapya Kombe la Muungano 2025
YANGA Mabingwa Wapya Kombe la Muungano 2025
Klabu ya Yanga SC ndio Mabingwa Wapya wa Kombe la Muungano 2025.
Klabu hiyo imefanikiwa kubeba Kombe hilo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU SC ya Zanzibar Katika mchezo wa Fainali uliochezwa Leo May 01,2025 kwenye Uwanja wa Gombani, Visiwani Zanzibar.
Bao hilo la ushindi limefungwa na Max Nzengeli Katika dakika ya 45.

YANGA Mabingwa Wapya Kombe la Muungano 2025
JKU SC ambao wamemaliza Katika Nafasi ya pili wamezawadiwa Tsh Million 30, huku Yanga wakibeba Kombe, Medali na Tsh Million 50.
Hilo linakuwa Kombe la 7 Kwa Yanga ikiwa ndiye Kinara akifuatiwa na Simba SC mwenye Makombe 6 ya Kombe la Muungano tangu lianzishwe.
Maxi Nzengeli ndiye Mfungaji Bora wa Mashindano haya na Mchezaji Bora wa Mchezo wa Fainali.
Mudathir Yahaya ndiye MVP wa kombe la Muungano 2025.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
